December 7, 2016



Kocha  wa zamani wa Simba, Selemani Matola ametajwa kuwa kocha mpya wa Ndanda FC ya Mtwara na ataanza kuiongoza timu huyo kwenye mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara.

Matola ambaye msimu uliopita alikuwa akiinoa Geita Gold Sport ya mkoani Geita iliyokuwa Ligi Daraja la Kwanza, aliamua kuachana nayo kutokana na kukumbwa na kashfa ya upangaji matokeo hali iliyosababisha kushushwa daraja.
Chanzo cha habari kutoka ndani ya Ndanda, kimesema Matola tayari ameshamalizana na timu hiyo, kinachosubiriwa ni kuanza kazi tu.

“Matola ameshasaini mkataba wa kuifundisha Ndanda na tayari ameshakuja huku zaidi ya mara mbili na kutoa mapendekezo ya wachezaji anaotaka wasajiliwe, hivyo mzunguko wa pili ukianza yeye ndiye ataiongoza timu.

“Alikuwa kwenye mazungumzo na viongozi kwa muda mrefu, katika mechi zile za kumaliza mzunguko wa kwanza alikuwa anakuja mara kwa mara kwa ajili ya mazungumzo hayo,” kilisema chanzo hicho.


Alipotafutwa Matola kuzungumzia taarifa hizo, hakupatikana lakini Ofisa Habari wa Ndanda, Idrissa Bandari, alisema: “Bado sijazipata taarifa hizo, labda zipo kwa viongozi wenzangu, lakini kesho (leo) ndiyo tutaweka bayana kila kitu kuhusiana na mikakati yetu ikiwemo ishu ya kocha.”

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic