Mshambuliaji nyota wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo amefunga bao lake la 500 wakati Real Madrid ikishinda kwa mabao 2-0 katika mechi ya Kombe la Dunia kwa upande wa klabu.
Madrid imeishinda Club America ya Mexico katika mechi hiyo ya Kombe la Dunia kwa klabu kwenye Uwanja wa Nissan nchini Japan.
Ronaldo alifunga bao la pili baada ya Karim Benzema kufunga la kwanza.
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 31 sasa alishinda tuzo ya Ballon d’Or 2016, Jumatatu iliyopita.









0 COMMENTS:
Post a Comment