December 9, 2016



Simba imeifunga Polisi Morogoro kwa mabao 2-0 katika mechi ya kirafiki kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini hapa.

Mabao ya Simba yalifungwa na viungo wake Abdi Banda na Ibrahim Ajibu huku wakifanikiwa kuonyesha kwamba kama wataendelea na maandalizi vizuri, watakuwa fiti zaidi.

Katika mechi hiyo, kipa mpya wa Simba, Daniel Agyei raia wa Ghana alidaka kwa dakika zote 90.

Lakini kiungo James Kotei raia wa Ghana, naye akaingia kuchukua nafasi ya Yassin Muzamiru huku wakiingia kwa pamoja na Jonas Mkude aliyechukua nafasi ya Said Ndemla.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic