December 1, 2016
Kiungo mkabaji, Justice Zulu raia wa Zambia ambaye ametua nchini kumalizana na Yanga, amesema atakuwa fiti baada ya siku chache na wao Yanga watafurahi.

Zulu anajiunga na Yanga baada ya kuwa amekaa nje kwa kipindi cha zaidi ya miezi minne bila ya kucheza baada ya kukumbana na adhabu ya Fifa, akituhumiwa ‘kumzika’ wakala wake.

“Amesema atakuwa fiti hasa baada ya muda mfupi ingawa alishaanza mazoezi ya kujifua mwenyewe kabla ya kuja nchini,” kilieleza chanzo.


Ujio wa kiungo huyo, unaonekana wazi kuwa unahitimisha kuwepo kwa Mbuyu Twite, beki kiraka wa Yanga ingawa kuna mjadala mambo yanaweza kubadilika na Zulu akachukua nafasi ya Vicent Bossou.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV