January 7, 2017



Simba SC imekiri kwamba baada ya kuona mastraika wao ni butu, ikaamua kuwapa mbinu viungo wao na ndiyo maana sasa wanafunga na hilo wala siyo tatizo kwao na ipo siku hata kipa atafunga.

Katika mechi za hivi karibuni za Simba iwe Ligi Kuu Bara hata kwenye Kombe la Mapinduzi linaloendelea huko Zanzibar, viungo washambuliaji wake ndiyo waliofunga mabao mengi kuliko mastraika.

Viungo hao ni Mzamiru Yassin na Mohammed Ibrahim ‘Cabaye’ ambapo wachezaji hao wamehusika katika ushindi wa mechi tatu za timu hiyo dhidi ya Ruvu Shooting (ligi kuu) na Jang’ombe Boys na KVZ katika Kombe la Mapinduzi.

Mayanja amesema kuwa, haijalishi mabao yao yanafungwa na viungo au mabeki bali wao wanachojali ni ushindi na suala hilo linaonyesha kwamba timu yao inamtegemea kila mchezaji.

“Kwanza watu wanatakiwa kuelewa kwamba timu inacheza kwa ushirikiano na kila mmoja ana haki ya kufunga pale atakapopata haijalishi ni beki au kipa ilimradi tupate ushindi.

“Hiyo ni mbinu ambayo tuliwafundisha wachezaji tangu zamani baada ya kuona fowadi yetu haina makali sana na pia hatukuwa tunataka kumtumia mchezaji mmoja pekee kwenye kufunga.


“Tunashukuru kwamba mbinu hiyo inafanya kazi na ndiyo inayotupa ushindi kwenye mechi zetu, hatujali kwamba tunapata ushindi mdogo na viungo wetu ndiyo wafungaji wa mabao badala yake sisi tunafurahia ushindi na tunaamini kwamba kwa staili hiihii tutaweza kutwaa makombe mengi,” alisema Mayanja.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic