January 7, 2017




Aliyekuwa Kocha wa Taifa Stars, Charles Boniface Mkwasa analidai Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Sh milioni 80 ikiwa ni fedha za malipo ya mshahara wake ambazo hajalipwa kwa miezi kadhaa.


TFF imeamua kuachana na Mkwasa hivi karibuni kwa makubaliano kufuatia mkataba wake kutarajia kufikia tamati Machi, mwaka huu kisha kumteua Salum Mayanga kushika nafasi yake hiyo.


Mayanga aliyekuwa akiifundisha Mtibwa Sugar, ana jukumu la kuandaa kikosi kitakachowania kufuzu Kombe la Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (Chan) Aprili mwaka huu.

Mshahara wa Mkwasa kwa mwezi ulikuwa Sh milioni 28 ambao aliurithi kutoka kwa Mart Nooij ambaye alisitishiwa mkataba kutokana na TFF kutoridhishwa na utendaji wake.

Akizungumza, bosi mmoja wa TFF alisema, Mkwasa anadai Sh milioni 80 ambazo anatarajiwa kulipwa kwa mikupuo miwili ndani ya mwezi huu.

“Ni kweli Mkwasa anaidai TFF Sh milioni 80 ambazo zinatokana na malipo ya mshahara wake ambao ulikuwa ukilimbikizwa, hivyo TFF ipo katika hatua za kumlipa fedha zake hizo kabla ya kocha mpya kuanza kazi.

“Fedha hizo zinatarajiwa kulipwa kwa mikupuo miwili ndani ya mwezi huu ambapo atalipwa katikati ya mwezi na mwishoni mwa mwezi,” alisema bosi huyo.


Alipotafutwa Ofisa Habari wa TFF, Alfred Lucas, alisema kwa kifupi: “Hayo ni mambo binafsi ya mkataba, hayafai kuwekwa wazi.”

SOURCE: CHAMPIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic