January 18, 2017Uongozi wa Azam FC umetamka kwamba utafanya kila linalowezekana kuendeleza makali yao waliyoyaonyesha katika Kombe la Mapinduzi kwenye michezo yao ya ligi wakianza kufanya hivyo leo dhidi ya Mbeya City.

Kikosi hicho cha Azam kinachofundishwa na Mromania, Aristica Cioaba kilifanikiwa kutwaa ubingwa wa Mapinduzi visiwani Zanzibar kwa kuwafunga Simba bao 1-0, ambapo leo Jumatano watawavaa Mbeya City katika Uwanja wa Azam Complex, Dar.

Msemaji wa timu hiyo, Jaffar Idd amesema kuwa tayari wamejipanga kuona wanaondoa matokeo mabaya waliyokuwa nayo kwenye mechi zao za nyuma kwa kuhakikisha wanacheza kwa kiwango cha juu kama walivyofanya Zanzibar.

“Tumepania kwamba matokeo mabaya tuliyokuwa nayo kabla kwenye mechi zetu za ligi yanabaki historia kwa kujipanga na kuibuka upya huku tukitaka kumaliza mechi zetu tukipata matokeo mazuri.


“Hilo tumelifanyia kazi na tutaanza kulionyesha leo tutakapowavaa Mbeya City ambapo timu ina morali kubwa ya kuona kwamba inapata ushindi kwa ajili ya kurudi kwenye mstari wake baada ya kupepesuka kwenye mechi za awali,” alisema Idd.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV