January 18, 2017




Baada ya Yanga kufanya vibaya kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi iliyomalizika hivi karibuni, Katibu wa Baraza la Wazee la Yanga, Ibrahim Akilimali, ameuomba uongozi wa klabu hiyo kuliangalia kwa umakini suala la kutofautiana kwa kocha mkuu, Mzambia, George Lwandamina na Mkurugenzi wa Benchi la Ufundi, Mholanzi, Hans van Der Pluijm.

Hivi karibuni, baada ya Yanga kuondoshwa na Simba hatua ya nusu fainali ya Kombe la Mapinduzi, kuliibuka madai kwamba Pluijm amekuwa hana uhusiano mzuri na kocha huyo raia wa Zambia hali ambayo ilipelekea Mholanzi huyo kutakiwa kuondoka.


Akilimali alisema kuwa uongozi wa juu wa klabu hiyo unapaswa kuliangalia kwa umakini suala la makocha hao kwani linaweza kuwa sababu kubwa ya timu kufanya vibaya.


"Kiukweli hili suala la Lwandamina na Pluijm uongozi niombe uliangalie kwa umakini mkubwa kwa sababu nijuavyo ni kwamba mafahari wawili hawawezi kukaa zizi moja na hilo lipo wazi, sasa lazima zichukuliwe hatua kwa manufaa ya timu.


"Unajua wakati Pluijm alipokuwa kocha wa Yanga hakuwa na rekodi mbaya kabla ya kupewa cheo kingine, sasa kibinadamu lazima awe na kinyongo na mwenzake, unadhani atakuwa anatoa ushauri sawasawa, ukiangalia hata wachezaji bado wanampenda, niwaombe sana viongozi wangu kuliangalia hili ili tuweze kutetea ubingwa wetu na siyo tufanye malumbano, tunataka turudishe umoja wetu kama zamani," alisema Akilimali.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic