Charles Boniface Mkwasa rasmi anaanza kazi kesho katika nafasi yake ya Katibu Mkuu mpya Yanga.
Mkwasa anakuwa mchezaji mwingine wa Yanga baada ya Lawrance Mwalusako kushika wadhifa huo wa utendaji.
Wakati akiwa mchezaji, alikuwa kiungo nyota wa Yanga na timu ya Taifa Stars.
Yanga inatarajia kumtangaza leo na Mkwasa atachukua nafasi ya Baraka Deusdedit aliyekuwa akikaimu nafasi hiyo ambaye imeelezwa anashushwa na kuwa bwana fedha.
Awali ilionekana, huenda Baraka angechukua nafasi hiyo na kuwa katibu kamili wa Yanga, hata hivyo ikaonekana hakuwa amefanya utendaji katika kiwango kilicho sahihi kama ambavyo uongozi wa Yanga ulitarajia.
0 COMMENTS:
Post a Comment