January 3, 2017


Kocha Joseph Omog ameanza kuyafanyia kazi yale yaliyojitokeza katika mechi dhidi ya Taifa Jang’ombe.

Simba inashuka dimbani katika mechi yake ya Mapinduzi Cup kuwavaa KVZ mjini Zanzibar.

Katika mechi hiyo ya kwanza ya Simba katika Kombe la Mapinduzi, pamoja na kushinda kwa mabao 2-1, lakini bado ilikosa nafasi nyingi za kufunga.

Meneja wa Simba, Mussa Hassan Mgosi amesema Omog ameyafanyia kazi yote yaliyoonekana ni tatizo.

“Soka mnajifunza kila kukicha, mazuri mnayaongezea na mabaya yanarekebishwa. Kocha ameyafanyia kazi.

“Imani yetu ni kufanya vizuri zaidi katika mechi ya leo na kikubwa ni mashabiki, watuunge mkono wakiamini tumelenga kufanya vema,” alisema.


Katika mechi hiyo ya kwanza, Simba ingeweza kushinda mabao zaidi kama ingekuwa makini lakini kuna kipindi ilipwaya katika sehemu ya kiungo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV