January 3, 2017





Kocha wa Yanga, George Lwandamina amefurahishwa na kikosi chake kushinda mabao 6-0 dhidi ya Jamhuri katika mechi ya Kombe la Mapinduzi mjini Zanzibar, jana.

Lakini amewataka wachezaji wake kuendeleza moto huo kwa kila timu kwa kuwa wana uwezo wa kufanya hivyo.

“Unajua mwanzo kocha alisema anataka kuona tunazitumia nafasi. Alionekana hana furaha na namna mwendo ulivyokuwa wa kupoteza nafasi,’’ alisema mmoja wa wachezaji nyota wa Yanga.

“Kwa wachezaji wengi tuna uchu wa kufunga, ndiyo maana aliposema kocha watu tukaambiana ni kuhakikisha tunafunga kweli nafasi ikipatikana.”


Yanga ilionyesha soka safi wakati ikiitwanga Jamhuri hiyo jana. Kabla ya hapo, ilikuwa ikipoteza nafasi nyingi hali iliyomfanya Lwandamina kuwaambia wachezaji lazima wawe makini na kuzitumia.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic