January 1, 2017


Benchi la ufundi la Yanga linaonekana kutoridhishwa na mabao yanayofungwa licha ya kwamba kikosi chao kinaongoza kwa ufungaji wa mabao.

Katika mechi 18 Yanga imefunga mabao 39 na ndiyo inayoongoza kwa kufunga katika timu zote za Ligi Kuu Bara.

Lakini Lwandamina amewaambia wachezaji wake anataka mabao zaidi na wanaweza kuanza kuonyesha kwenye michuano ya Mapinduzi.

“Kocha kasisitiza sana suala la kutumia nafasi. Mechi na Lyon tulipoteza nafasi nyingi sana, tukaambulia sare. Mechi na Ndanda umeona tumerudi na kocha anataka hivyo au zaidi,” alisema mmoja wa wachezaji wa Yanga.


Benchi la ufundi, bosi mkuu ni Hans van der Pluijm ambaye ni mkurugenzi wa ufundi, kocha mkuu ni George Lwandamina raia wa Zambia.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic