Mshambuliaji wa Simba, Ibrahom Ajib kwa
kiasi kikubwa
amekonga nyoyo za mashabiki wa Haras El Hodood ya Misri baada ya kucheza
mechi yake ya kwanza ya kirafiki na kufunga bao.
Awali, Haras el Hodood waliwaambia Simba
jana Desemba 31, 2016 ndiyo siku ya mwisho ya majaribio. Maana yake jibu
linatakiwa kutolewa leo.
Lakini kwa upande wa wachezaji wenzake
wameonyesha kuvutiwa naye kutokana na namna alivyokuwa msaada katika mechi hiyo
ya kirafiki waliyoshinda kwa mabao 4-0.
Katika picha mbalimbali zilizozagaa
mitandaoni, Ajibu ameonyesha kuwa karibu na wachezaji wenzake licha ya kuwa
mgeni.
Awali, uongozi wa Simba ulisema, Ajibu alifuzu vipimo vya afya na ilikuwa limebaki suala la benchi la ufundi kutoa
uamuzi.
Haras El Hodood ambao walipomoroka hadi
daraja la kwanza, inatarajiwa kutoa jibu leo au kesho kuhusiana na Ajibu.








0 COMMENTS:
Post a Comment