January 4, 2017Zikiwa zimebaki wiki mbili pekee kabla ya kuanza kwa Michuano ya Kombe la Mataifa Afrika (Afcon), beki wa Yanga aliye na kikosi cha timu ya taifa ya Togo, Vincent Bossou ameweka bayana kwamba atapigana kwenye kombe hilo kuhakikisha kwamba anaitangaza timu yake.

Bossou ni miongoni mwa wachezaji watatu watakaoiwakilisha Ligi ya Tanzania Bara kwenye mashindano hayo yatakayofanyika nchini Gabon kuanzia Januari 14 wengine ni Bruce Kangwa wa Azam na Juuko Murshid wa Simba ambapo Togo imepangwa kundi C, ikiwa na timu za Morocco, Ivory Coast na DR Congo.

Akizungumza kutoka Senegal kilipo kikosi hicho kwenye kambi yake amesema kwamba:

“Nipo huku Senegal kabla ya kwenda Gabon kushiriki Afcon, niwaambie mashabiki wa Yanga na Tanzania kwa ujumla kuwa nimepanga kuonyesha kiwango kama nilivyokuwa huko kwa ajili ya kuitangaza ligi ya Bongo watu wanifuatilie waone moto wangu.


“Najua hilo nitalifanikisha kwa sababu nipo vizuri na bado nina kiwango kilekile nilipokuwa huko na tunaamini kwamba tunaweza kufanya vizuri katika mashindano haya kwa sababu tuna kikosi kizuri licha ya kwamba tupo kwenye kundi gumu,”alisema Bossou.

SOURCE: CHAMPIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV