January 4, 2017

COASTAL UNION (MSIMU ULIOPITA)

Baada ya Coastal Union kufanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 4–1 dhidi ya Kimondo FC kwenye Uwanja wa Karume jijini  Dar, kocha wa timu hiyo, Mohamed Kampira ameibuka na kusema anatamani mechi zao zote za nyumbani zilizosalia wamalizie uwanjani hapo.


Mchezo huo wa Kundi B, ulipangwa kuchezwa uwanjani hapo ikiwemo ni sehemu ya adhabu kwa Coastal Union kucheza mechi moja nje ya uwanja wao wa nyumbani wa Mkwakwani na mbili kucheza hapo bila ya mashabiki baada ya mashabiki wake kumpiga mwamuzi walipocheza dhidi ya KMC.

Kocha huyo alidai kuwa, wanapocheza nje ya Mkwakwani ndiyo wanacheza vizuri zaidi na kupata matokeo mazuri tofauti na wanapocheza nyumbani.

“Tangu msimu huu uanze, hatujawahi kushinda wala kupata sare katika uwanja wetu wa nyumbani, tumefungwa na Polisi Morogoro, KMC na Njombe Mji, lakini tukicheza nje ya tunapata matokeo mazuri.

“Nadhani uwanja wetu wa nyumbani tunafanya vibaya  kutokana na presha ya mashabiki wetu kutaka matokeo ya haraka kiasi cha kusababisha wachezaji kushindwa  kucheza kwa kufuata maelekezo, hivyo ni bora mechi zetu zote za nyumbani tuchezee katika Uwanja wa Karume, Dar,” alisema Kampira.

Coastal Union kwa sasa inashika nafasi ya sita ikiwa na pointi tisa, huku KMC ikiongoza kundi hilo ikiwa na ponti 19.

SOURCE: CHAMPIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV