January 4, 2017Siku chache baada ya Mkurugenzi wa Ufundi wa Yanga, Mholanzi, Hans van Der Pluijm kudaiwa kuwa yupo mbioni kutaka kujiunga na timu ya Azam, uongozi wa klabu hiyo umesema hana sifa hizo.

Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Saad Kawemba amesema kuwa Pluijm hana sifa kwani kocha wanayemhitaji ni yule ambaye ameshafika fainali kwenye michuano mikubwa Afrika.

Alisema baada ya kuondoka kwa Mhispania, Zeben Hernandez sasa hawawezi kurudi tena nyuma kwani wanataka kufika mbali zaidi.

 “Kama Pluijm anazo sifa hizo basi tutampatia ajira hiyo lakini kwa jinsi tunavyofahamu sisi hana sifa hizo, hivyo hawezi kuwa kocha wa Azam hata huyo Charles Mkwasa ambaye naye hivi karibuni amehusishwa kuwa tunamtaka hana sifa.


“Nichukue nafasi hii kusema kuwa makocha hao hatuna mpango nao kwa sababu hawana sifa za kocha tunayemtaka kwa ajili ya kuja kuifundisha timu yetu,” alisema Kawemba.

SOURCE: CHAMPIONI

2 COMMENTS:

  1. Watahangaika sana azam, nadhani wanapaswa kubadili fikra zao, hivi wanakumbuka walimwacha Omog mwenye sifa kama hiyo? Walidai eti ameshindwa kutimiza malengo ya kuifikisha azam mbali kwenye michuano ya club bingwa Africa huku akiwa ni mwaka wa kwanza tu wa mkataba. Hivi wanadhani mafanikio ya tp mazembe, na timu za waarab ni ya uwekezaji wa mwaka mmoja tu? Miaka 9 makocha 9 naamini tatizo ni management na si kocha kama wanavyojaribu kutuaminisha. Hata aje Guardiola azam haitabadilika mpaka management iamue kujitahmini yenyewe na kubadilika."Azam imekuwa kama mpishi anayelaumu mkulima kuwa Hana sifa za kupika chakula kitamu kumbe yeye mwenyewe si hodari na hajui kupika"

    ReplyDelete
  2. pole sana wewe Kawemba. inaonekana hata mpira hujaufahamu sana. sasa huoni unajidanganya mwenyewe kwa kauli zako??? kaka unapotoa kauli kama mtendaji wa klabu unatakiwa kukumbuka mambo mengi ya mpira. kumbuka mwanzoni mlipowasajili hao wahispain mlisema kazi yenu si kutaka ubingwa ila ni kujenga timu kwa ajili ya baadae, sasa hiyo mipango imetimia?? au hao wa hispain walikuwa na sifa mlizozitaka?? kama walikuwa nanzo je wametimiza malengo mliyoyataka kitimu?? eti akina mkwasa na Pluijm hawana sifa, sasa huyo Ongalla ana sifa za kupewa timu kwa muda mfupi??
    unakosea kaka, makocha hawa ni wazuri wakipewa mikataba itakayowabana.
    ni mawazo tu

    ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV