January 4, 2017

TWITE AKIWA NA MAKAMU MWENYEKITI WA FANYA, INJINIA SEIF AL SUMRI ALIYEMPOKEA MJINI MUSCAT, OMAN.


Beki Mbuyu Twite amejiunga na Fanja FC ya Oman, amesaini mkataba wa miaka miwili.

Mtanzania mwingine anayeichezea Fanja ni mshambuliaji Danny Lyanga wa Simba ambaye yuko kwa mkopo katika kikosi hicho.

Twite amejiunga na timu hiyo kongwe ya Oman baada ya uongozi wa Yanga kuamua kuachana naye ili nafasi yake itumiwe na Justice Zulu raia wa Zimbabwe.

Twite raia wa DRC aliyewahi kuchukua uraia wa Rwanda, ana uwezo mkubwa wa kucheza nafasi zaidi ya moja uwanjani.


Sifa nyingine kubwa ya Twite aliyewahi kung’ara na APR ya Rwanda ni uwezo mkubwa wa kurusha mbali, mipira ya kurusha.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV