| SIKU ALIPOONDOKA... |
Farid
Mussa amewasili katika visiwa vya Cannaries nchini Hispania tayari kuanza kazi
katika kikosi cha Tennerife.
Timu
hiyo ipo katika kisiwa cha Tenerife ndani ya visiwa hivyo vya Cannaries ambavyo
viko karibu kabisa na nchi ya Morocco, Kaskazini mwa bara la Afrika.
Jose
Thomas, mmoja wa viongozi wa mashabiki wa timu hiyo amesema Farid amepokelewa.
“Ndiyo
amepokelewa, lakini sijafika kuona mechi wala mazoezini. Lakini ninaamini
atakuwa ameanza kazi na kama bado basi baada ya mwaka mpya ataanza,” alisema.
Farid
alichelewa kwenda Hispania kuanza kazi kwa madai ya kukosa kibali ingawa
inaelezwa hakukuwa na suala la maelewano vizuri kati ya mawakala waliompeleka.







0 COMMENTS:
Post a Comment