January 4, 2017Simba imesema bado inasubiri taarifa kutoka Haras El Hodood na Ibrahim Ajibu bado ni mchezaji halali Simba.

Awali kulikuwa na taarifa zinazozagaa mitandaoni kuonyesha El Hodood ya Misri wamekamilisha usajili wa Ajibu.

Makamu Rais wa Simba, Geofrey Nyange Kaburu amesema taarifa hizo, hazina ukweli.

"Haziwezi kuwa na ukweli, hawawezi kumsajili mchezaji bila ya mawasiliano nasi.

"Ajibu amerejea tokea juzi, lakini bado tunaendelea kusubiri kutoka kwa Haras El Hodood," alisema.

Alisema Ajibu ataungana na wenzake Zanzibar ambako timu hiyo inashiriki michuano ya Mapinduzi na kuendelea na majukumu.

Ajibu alipewa ruhusa ya siku 10 kufanya majaribio katika timu hiyo katika mji wa Alexandria nchini Misri.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV