January 3, 2017Simba imeshinda mechi yake ya pili katika Kombe la Mapinduzi baada ya kuitwanga KVZ kwa bao 1-0.
Shujaa wa Simba ni Muzamiru Yassin aliyefunga bao katika dakika ya 43 baada ya kuutegua mtego wa kuotea wa mabeki wa KVZ.

Hata hivyo, KVZ ilionyesha soka safi na la kuvutia na kuwapa Simba wakati mgumu.

Washambuliaji wa Simba, Juma Luizio na Pastory Athanas walipata nafasi nyingi za kufunga lakini wakashindwa kuzitumia.

Shiza Kichuya naye alipata nafasi mbili nzuri za kufunga katika dakika za mwisho kipindi cha pili, lakini hakutumia nafasi hizo.

Samba walicheza kwa kushambulia kwa kushitukiza lakini suala la umaliziaji liliendelea kuonekana halina uhakika.

Mechi ya kwanza, Simba iliishinda Taifa Jang’ombe kwa mabao 2-1.


Ushindi huo kwenye Uwanja wa Amaan, bado ilionekana mashabiki wa Simba kutokuwa na furaha sana ikionekana wazi walitaka kuona timu yao ikishinda kwa mabao mengi zaidi, jambo ambalo halikutokea.

Mwishoni zikiwa zimebaki dakika mbili, beki wa KVZ alilambwa kadi nyekundu kwa kumvuta jezi Pastory akienda kufunga. Lakini bado Simba hawakuweza kuitumia vizuri nafasi hiyo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV