January 10, 2017




Mechi ya watani Simba Vs Yanga inapigwa leo na hilo ndiyo gumzo la kila sehemu hasa unapozungumzia mchezo wa soka.
Simba inaivaa Yanga katika mechi nusu fainali ya ya Kombe la Mapinduzi kwenye Uwanja wa Amaan mjini Zanzibar.

Mara nyingi mashabiki wa soka wanakuwa ni watu wanaoamua wanachokiamini hata kabla mpira haujachezwa.

Wengi sana wamekuwa wakiamini Yanga itapoteza mchezo huo, kinachowafanya waamini Yanga itapoteza ni kwa kuwa tu ilifungwa mabao 4-0 dhidi ya Azam FC katika mechi iliyopita.

Hilo ni kosa kubwa sana kwa kuwa Yanga imepoteza lakini ndiyo timu iliyokuwa inafanya vizuri zaidi ya timu nyingine.

Kabla ya kufungwa na Azam FC, Yanga iliitwanga Jamhuri kwa mabao 6-0, halafu wakaifunga Zimamoto 2-0 kabla ya kukutana na gharika ya Azam FC.

Utaangalia kawa kabla, safu ya ulinzi ya Yanga katika mechi mbili haikuwa imeruhusu bao, ikafanya makosa na ikaruhusu mabao manne katika mechi moja.

Katika mechi mbili, Yanga walikuwa wamefunga mabao nane na kuwa wenye mabao mengi zaidi ya timu nyingine, katika mechi hiyo moja dhidi ya Azam wakashindwa kufunga.

Yanga ina wachezaji wazoefu na wanaoujua mpira hasa ukizungumzia kwa kiwango cha soka hapa nchini. Maana yake wana nafasi kubwa ya kujirekebisha wakiyatumia makosa dhidi ya Azam FC.

Kama wana uwezo wa kujirekebisha, maana yake kuna nafasi kubwa sana ya kufanya vizuri.

Simba wana kikosi kizuri ambacho wamekuwa makini sana. Licha ya ushindi wa bao chache lakini wanaonekana ni wenye malengo na wamejipanga wanataka nini.

Kikubwa cha kuamini kuwa mchezo wa leo ni mgumu hasa kwa kila timu na kila mmoja lazima awe makini sana.


Simba wanataka kuendeleza ushindi wa mechi zote kama walivyoanza, Yanga wanataka kujirekebisha na huenda ndiyo wakawa hatari zaidi kwa kuwa hawatakubali kufungwa mara mbili.

2 COMMENTS:

  1. Yanga physically wanaweza wakaonekana kupata ushindi, Ila inapofikia mtanange wa baina ya hizi timu mbili Yanga anafungwaga kutokana na kuwa dhaifu mentally. Pamoja mi ni mshabiki wa Yanga ila inapofikia mechi kati timu hizi mbili hasa ukiongelea kwa sasa Yanga hawapo vizuri pamoja na kushinda mechi zao zilizo tangulia

    ReplyDelete
  2. Ili yanga iifunge simba, itabidi wapatiwe yule refa alieruhusu bao la Tambwe la mkono na kumpa Mkude kadi nyekundu ambayo ilibatilishwa baadae

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic