January 10, 2017
MPIRA UMEKWISHAAAAA
DAKIKA 3 ZA NYONGEZA
Dk 89, Mavugo anaingia na kuachia shuti hapa, lakini shuti mtoto
Dk 88, Muzamiru anaingia vizuri lakini shuti lake linakuwa halina nguvu, Dida anadaka
SUB Dk 85 Simba wanamwingiza Mavugo kuchukua nafasi ya Mo Ibrahim aliyeumia

Dk 83 Simba wanachonga kona nyingine lakini Dida anafanyiwa madhambi hapa
Dk 82 Simba wanapata kona nyingine baada ya Mwinyi kuokoa, inachongwa, inachongwa hapa, kona tena.
Dk 81 Mo Ibrahim anageuka vizuri na kuachia shuti kali hapa, goal kick
Dk 80, Mkude anatolewa nje kwenda kutibiwa baada ya kugongana na Bukungu

Dk 78, Martin anawatoka Mkude na Bukungu wanaogongana na yeye anaachia mkwaju mkali hapa. Agyei anaonyesha umakini na kudaka vizuri hapa
SUB Dk 77, Simba wanamtoa Luizio nafasi yake inakwenda kwa Pastory Athanas
Dk 76, mpira bado unachezwa sana katikati ya uwanja na Yanga wanaonekana kuanza kukontrooo mpira zaidi ya Simba
Dk 71, Msuva anaingia vizuri lakini mpira wake wa krosi unaokolewa na Bukungu
Dk 69, nafasi nyingine kwa Simba, lakini Luizio anashindwa kupiga krosi nzuri
Dk 68, Yanga wanachonga kona safi, kichwa cha Mwinyi mpira unakwenda nje

Dk 65 sasa, bado mpira unachezwa katikati ya uwanja zaidi
SUB Dk 62 Yanga wamatoa Kaseke na nafasi yake inachukuliwa na Emmanuel Martin
Dk 61 sasa, mpira bado unachezwa katikati ya uwanja zaidi
Dk 55, kosa hapa Dante anachichanganya Simba wanaingia hatariiiiiii Dante anaokoa
Dk 54, kona ya Kichuya, hatari tena, Dida anaokoa hapa
Dk 53, Kichuya anaingia vizuri hapa, hatariiii lakini Dante anamuwahi na kutoa nje, kona
Dk 53, Juma Abdul anacheza faulo hapa lakini mwamuzi anamsamehe, akimuonya kwa maneno. Kumbuka kadi ya njano


Dk 52 kona nyingine inachongwa na Kotei lakini Yanga wako makini wanaokoa
Dk 51, Simba wanafanya shambulizi kali hapa, krosi ya Kichuya Yondani anaokoa na kuwa kona, inachongwa na Kichuya, Dida anaokoa tena na kuwa kona tena
Dk 49, Simba wanagongeana vizuri na Mo Ibrahim anaachia mkwaju na Dida anadaka vizuri
Dk 47 krosi nzuri ya Mwinyi lakini Mwanjale anauwahi, kona. Inachongwa na Niyonzima , wanaokoa
Dk 46, Yanga wanacheza vizuri, lakini Tambwe anashindwa kupiga krosi kutokana na kasi ya mpira
Dk 45, Kipindi cha pili kimeanza na inaonekana suala la hofu kwa wachezaji bado limejaa
MAPUMZIKO
KADI Dk 45, Mwamuzi anatoa kadi ya njano kwa Abdi Banda kumuangusha Kaseke, kadi ya njano kwa Juma Abdul
Dk 43, hatariiiii, Msuva anapoteza mpira, Mo Ibrahim anaachia fataki, Dida anaugusa na kutgonga mwamba, unamkuta Luizio anaachia shuti, goal kick
Dk 40, Banda anaachia fataki lakini mpira unawagonga mabeki wa Yanga, wanaokoa
KADI Dk 39, Mwingi analambwa kadi ya njano kwa kumrukia Mo Ibra

Dk 37, Msuva anamtoka Zimbwe kwa mara ya kwanza, anaingia vizuri na kujaribu kupiga lakini mpira anaukosa na Bukungu anauokoa kabla haujavuka lango

Dk 34, Dida anafanya kosa hapa, nusura Bukungu lakini anaitahi kuuwahi

Dk 34 mechi bado inaonekana kuwa ngumu, kila upande una mashambulizi lakini si uhakika

Dk 28, Yanga inapata kona baada ya Simba kuukoa mpira wa faulo wa Mwinyi, inachongwa lakini kipa anafanyiwa madhambi
Dk 21 sasa, mambo bado, mashambulizi si mengi. Simba hasa Banda wanapaswa kuwa makini na kupunguza mipira isiyokuwa na maana karinu lango lao
Dk 18, mkwaju mkali wa Mwinyi wa faulo, unatoka kidogo nje ya lango la Simba
Dk 16, Mo Ibrahim, anaachia shuti kali katikati ya msimu wa mabeki wa Yanga, Dida anadaka vizuri kabisa

Dk 15, Yanga wanapoteza nafasi, Msuva anapiga shuti lakini Banda anakaa chini na kuzuia. Ilikuwa nafasi nzuri kwa Yanga

Dk 10 sasa, kila upande unaonekana kuwa makini sana kwa sababu hakuna mashambulizi mengi kwenye milango
Dk 8, Banda anapiga kichwa mpira unamkuta Niyonzima, anaingia vizuri na kuachia shuti kali hapa, Agyei anadaka vizuri kabisa

Dk 7, mpira zaidi unachezwa katikati ya uwanja ingawa Simba ndiyo wanaonekana kutawala zaidi katikati ya uwanja
Dk 3Yanga wanaanza kuwa wa kwanza kuingia kwenye lango la Simba lakini Mwanjale anakuwa makini

Dk 1Mechi imeanza kwa kasi kubwa huku ikionekana kila timu imepania kupata bao la mapema

3 COMMENTS:

 1. Jamani Manji Yuwapi? Hasikiki au ndio keshachoka na Yanga anaona pesa inaangamia bila ya faida?

  ReplyDelete
 2. This comment has been removed by the author.

  ReplyDelete
  Replies
  1. Ilikua ni mechi ya kawaida sana iliyokuzwa na mashabiki hasa wa Simba kwa kuamini kwamba wangeweza kushinda kwa margin kubwa baada ya Azam kuweka utelezi.........Kimantiki Yanga walicheza vizuri kiasi half ya kwanza japo concentration ilikua on and off hasa kwa play makers na full backs (Kaseke, Kamusoko, Mwinyi na Mnyamani) na utulivu uliwachanganya Simba ambao bila kujijua walijikuta wakiingia mtego wa kuwaiga Yanga na hivyo kupotea kabisa, High balls kawaida huchezwa na timu zenye rasilimali za kutosha kitu ambacho yanga wanacho (Msuva&Tambwe) na Simba hawana.......kitendo cha simba kutaka kucheza high balls ilikua ni ubatili na kujilisha upepo....naamini kabisa ungemuuliza mchezaji yeyote wa Simba kuhusu mechi ile asingekupa uhakika ambao mshabiki wa simba angekupa (kwa kujua madhaifu ya timu yao) kwani tangu kuanza kwa michuano hii mfuatiliaji wa makini atagundua kwamba Simba walikua mazoezini haswaaa ya kutafuta pattern mintaarafu kwenye safu ya ushambulizi thus huwezi kudanganyika ati kwa kuwa Azam waliifunga Yanga basi Simba wangalishinda kirahisi kwani uwezo wao ulikua wa kawaida sana kwa michezo yao wakionekana kabisa kukosa Team work hasa safu ya mbele......upande wa Yanga kipigo cha Azam kinaonekana kiliwatoa mchezoni na waliingia kitahadhari sana kuhakikisha w=hawafungwi ingawa kisaikolojia utaona kwamba walikua hawana matumaini ya kushinda pia japo kutokana na kuwa na kikosi kwa muda mrefu faida kubwa ingalikua kwao (licha ya mabadiliko ya kocha) ....hata hivyo hii ina maana kubwa sana kwa Simba wanaporusi kwenye ligi maana ari itakua juu zaidi na ina maana pia kwa Yanga kutuliza vichwa.........naamini kwa kuwa Simba imeshinda hata haya niliyoaandika ni ubatili maana haijalishi imeshindaje kwa maana hasa ya WATANI WA JADI

   Delete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV