January 10, 2017
Ligi Kuu ya soka ya wanawake ya Shirikisho la la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), inatarajiwa kuendelea kesho Jumatano Januari 11, 2017 kwa michezo sita katika viwanja mbalimbali nchini.

Kwa mujibu wa ratiba mechi hizo sita ni kwa kila kundi litakuwa na timu tatu. Michezo ya kundi ‘A’, itakuwa ni kati ya Mburahati Queens itacheza na Fair Play ya Tanga kwenye Uwanja wa Karume, Dar es Salaam.

Michezo mingine kwenye kundi hilo itakuwa ni kati ya Viva Queens ya Mtwara itakayokuwa mwenyeji wa JKT Queens ya Dar es Salaam kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona wakati Evergreen ya Temeke itakuwa mgeni wa Mlandizi Queens kwenye Uwanja wa Mabatini, Mlandazi mkoani Pwani.

Kundi B pia kutakuwa na mechi tatu ambako Baobab ya Dodoma itakuwa mwenyeji wa Majengo Queens ya Singida kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma wakati Panama ya Iringa itacheza na Marsh Academy ya Mwanza huko mjini Iringa huku Sisterz ya Kigoma ikiikaribisha Victoria Queens ya Kagera.


Mara baada ya michezo hiyo, ligi hiyo itaendelea tena Januari 18 kwa michezo minne katika makundi yote.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV