January 29, 2017


Kocha George Lwandamina amewata wachezaji wake kuondoa presha ya kuwaza kurejea kileleni na badala yake wacheze kwa lengo la kuishinda Mwadui FC, leo.


Yanga inakutana na Mwadui FC katika mechi ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, leo.


Iwapo Yanga itashinda, basi itapaa hadi kileleni ikiwa na pointi 46 na kuiacha Simba yenye 45 kileleni hadi sasa.


“Kocha kasisitiza suala la pointi tatu na si kuwenda kileleni. Ametuambia tunachotakiwa kufanya ni ushindi  kwa lengo la kupata pointi tatu.

“Ametukataza suala la kufikiria kukaa kileleni kwa kuwa linaweza kutupa presha na kushindwa kufanya vizuri dhidi ya Mwadui FC,” alisema mmoja wa wachezaji wa Yanga ambaye sasa ni tegemeo.


Imeelezwa Lwandamina anayesifika kwa uwezo mkubwa wa masuala ya saikolojia kwa wachezaji amegundua kuna presha kubwa ya wachezaji kuhusiana na kukaa kileleni na kuipita Simba.


Simba imebaki pengo la pointi mbili tu kati yake na Yanga baada ya jana kukubali kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Azam FC. 
0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV