January 19, 2017


Kocha George Lwandamina amewaambia wachezaji wake kuendelea kujiamini kwa kuwa mambo yatakaa sawa tu.

Lwandamina anaamini kikosi chake kilicho katika nafasi ya pili kikiwa na pointi 43 nyuma ya Simba yenye 45, kitakaa vizuri na kuwashangaza wengi.

“Hata hivyo kocha ametutaka kuwa watulivu katika kipindi cha mawimbi,” alisema mmoja wa wachezaji wakongwe wa Yanga.

“Katuambia ambas tunaweza kutuliza haya mawimbi ni sisi wenyewe na tunatakiwa kuwanza kutulia sisi kwanza ili mawimbi yatulie.”

Kumekuwa na presha kubwa upande wa Yanga hasa kwa mashabiki ambao wanaona kama Lwandamina hafanyi vizuri.


Lakini Yanga inaendelea kuonekana inapata kasi na kuhamisha presha hiyo kwa Simba.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV