January 30, 2017LYANGA AKIWA MAZOEZINI

Mtanzania Ayubu Reuben Lyanga tayari ameanza mazoezi na timu yake mpya ya Zanaco ya Zambia.

Mtanzania huyo amejiunga na timu hiyo akitokea African Sports ya Tanga na sasa ana nafasi ya kushiriki Ligi ya Mabingwa Afrika.

Meneja wa Lyanga, Jamal Kisongo amesema Lyanga ana nafasi nzuri ya kufanya vizuri.

“Tunaamini atafanya vizuri, bado ni kijana lakini ni mtu mwenye malengo hasa. Anajituma, msikivu na ndiyo maana sina hofu kuhusiana na suala la mafanikio,” alisema.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV