January 30, 2017


Msafara wa kikosi cha Mamelodi Sundowns FC ya Afrika Kusini umewasili leo Jumatatu mchana jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuweka kambi kwa muda kisha kucheza mechi mbili za kirafiki.

Mamelodi wamewasili Dar es Salaam wakiwa na jumlaya watu 42 huku ikielezwa kuwa wengine 10 wanatarajiwa kuingia kesho Jumanne.

Ikiwa Dar es Salaam, Mamelod inatarajiwa kucheza mechi za kirafiki dhidi ya Simba kwenye Uwanja wa Taifa kisha dhidi ya Azam FC kwenye Uwanja wa Azam Complex wiki hii kabla ya kuondoka Jumamosi ijayo.
0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV