January 7, 2017Nahodha wa Simba, Jonas Mkude amesema bado hawajakata tamaa ya kusonga mbele zaidi katika Kombe la Mapinduzi licha ya kutoka suluhu na URA na hawatajali wanapambana na timu gani.

Akizungumza baada ya mchezo dhidi ya URA juzi usiku kwenye Uwanja wa Amaan, Mkude alisema mechi hiyo ilikuwa ngumu kwao lakini sare waliyopata haijawakatisha tamaa.

 Mkude alikiri timu yake kupoteza nafasi mbili za wazi za kufunga, hivyo amesema watajipanga kuhakikisha hawafanyi makosa katika mchezo wao unaofuata katika michuano hiyo.

“Mchezo ulikuwa mzuri lakini pia ulikuwa mgumu na ndiyo maana tumeweza kutoka sare, hatujakata tamaa katika kuendelea na michuano hii na naamini tutafika mbali zaidi,” alisema Mkude.

Mbali na hilo, Mkude alisema watajipanga kuhakikisha wanafanya vizuri katika mchezo wao wa kesho Jumapili dhidi ya Jang’ombe Boys utakaopigwa saa 10:00 jioni kwenye Uwanja wa Amaan.


Simba hadi sasa ina pointi saba katika mechi tatu ilizocheza ambapo imeshinda mara mbili na kutoka sare moja ikiwa imefunga mabao matatu na imefungwa bao moja.

2 COMMENTS:

  1. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
  2. Nilichojifunza ni kwamba Simba inapokutana na timu ambayo haijawasoma mbinu yao ya kiungo, basi inatokea viungo wanakua free sana kusukumiza mashambiliz, kingine ni kwamba huenda ni kutokana na mazoea tu lakini wanaoitwa viungo Mzamiru na Mo kiasili wanaonekana ni washambulizi nyuma ya striker na wakipata kocha mzuri sana wa 442 watafunga zaidi, ukiwabana simba kiungo kisitembee umewamaliza kama walivyofanya URA.......zaidi ya yote ni ukweli kwamba Simba haijapata mpachika mabao wa asili inagwa huenda ukajenga hoja ya Mavugo kuwa mfungaji bora Burundi lakin ukumbuke alikua analishwa na sasa inabidi atafute na yeye (total football) na nimewaangalia Pastory na Liuzio bado sijawashika sana kama wana sifa ya upachikaji mabao ingawa wanaweza kuwa wasaidizi wazuri sana kwa wapachika mabao kutokana na kasi yao ....nahitimisha kwamba ni sahihi wanachofanya na kupanga simba kwa sasa kwani fimbo iliyo mkononi ndiyo huua nyoka

    ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV