January 5, 2017Kiungo mwenye kasi wa Yanga, Simon Msuva wa Yanga, amesema anautaka ufungaji bora na uchezaji bora wa Kombe la Mapinduzi.

Msuva amesema angependa kupata ufungaji bora wa michuano hiyo kwa mara ya pili. Kwa sasa anaongoza kwa kuwa na mabao manne ya kufunga.

“Kweli nataka ufungaji bora, niliwahi kuwa mfungaji bora wa Mapinduzi,” alisema.

“Kwa ushirikiano na wenzangu kwenye timu, ningependa kwua mfungaji bora. Kawaida ushirikiano unamsaidia mtu kuwa bora zaidi,” alisema.


Katika mechi mbili dhidi ya Jamhuri ambayo Yanga ilishinda kwa mabao 6-0 na ule dhidi ya Zimamoto, ikishinda mabao 2-0. Msuva alifunga mabao mawili kila mechi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV