January 5, 2017




Mfumo wa Kocha George Lwandamina umeanza kuwashitua baadhi ya wapinzani wa Yanga katika michuano ya Mapinduzi.
Yanga imekuwa ikitumia pasi ndefu za katikati ya uwanja kutengeneza mabao na inaonekana Thabani Kamusoko na Haruna Niyonzima ndiyo wamepewa jukumu hilo.

Wawili hao, wamekuwa wakipiga pasi ndefu kwa Amissi Tambwe, Donald Ngoma au Simon Msuva ambao wamekuwa wakimalizia pasi hizo.

Taarifa zinaeleza, ndani ya vikosi vya Simba na Azam FC, gumzo la mabao ya Yanga na pasi zinazopigwa limekuwa gumzo.

"Ni kweli, unaona kabisa kuna aina fulani ya kitu kinafundishwa. Tunajua na tunafuatilia. Haina maana tutacheza kama Yanga lakini lazima uwajue wapinzani wako mapema," alisema mmoja ya wahusika ndani ya Simba lakini akaomba kutotajwa jina.

"Kama mwenzako anafanya kazi vizuri, basi lazima ujifunze au uangalie unafanyaje vizuri zaidi yake au unaweza kumshinda."
Lakini upande wa Azam FC, John Bocco ambaye ni nahodha alisema wanaona kila kitu na wanajiandaa.

"Kweli kuna mambo mengi ya kujifunza kila unapocheza. Yanga ni timu kubwa, wamefunga mabao mengi lakini sisi tuna kikosi bora. Kina uwezo wa kupambana na kila mfumo," alisema.

Tayari Yanga imefuzu katika hatua ya mtoano baada ya ushindi mara mbili mfululizo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic