January 9, 2017Mshambuliaji wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo ametangazwa kuwa mwanasoka bora wa dunia wa tuzo za Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa).

Tuzo hizo zimefanyika jijini Zurich nchini Uswiss na Ronaldo ,31, amebeba tuzo hiyo huku akiwashinda mshambuliaji wa Barcelona na mpinzani wake mkubwa Lionel Messi na yule wa Atletico Madrid, Antoine Griezmann.

mwishoni mea mwaka jana yaani 2016, Ronaldo aliwashinda Messi na Griezmann na kubeba tuzo ya Ballon d’Or.


Ronaldo aliisaidia Real Madrid kubeba ubingwa wa Ulaya lakini akaisaidia Ureno kubeba ubingwa wa Ulaya kwenye euro 2016 nchini Ufaransa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV