January 7, 2017
MPIRA UMEKWISHA
-SUB Azam FC wamatoa Yakubu Mohammed na nafasi yake inachukuliwa na Kheri Mohammed 

DAKIKA 2 ZA NYONGEZA
Dk 90 Mwashiuya analambwa kadi ya njano kwa kumzuia Atta kwa mikono
Dk 88, Sure Boy anapoteza nafasi nyingine na mwamuzi anasema ni kona, inachongwa na Mahundi, Dida anadaka kwa ulaiiinii
SUB Dk 86, Azam FC wanamtoa Bocco na nafasi yake inachukuliwa na Mudathiri
GOOOOOO Dk 84, Atta anaifungia timu yake bao safi akiunganisha safi pasi ya Afful baada ya Mwashiuya kuukosa mpiraDk 82, Yanga na wanaonekana kuamka lakini ukiangalia hakuna matumaini
GOOOOOOOOO Dk 81, Mahundi anageuka, anatisha anauachia mpira upite mbele yake, anaachia fataki kali hapa, umbali wa mita 26 hivi na kuandika bao safi kabisa kwa Azam.
SUB Dk 79, Enock Atta Ageyi raia wa Ghana anaingia kuchukua nafasi ya Domayo
Dk 77, Azam FC wanafanya shambulizi kali hapa, Bocco anaachia mkwaju mkali lakini mpira unapiga nyavu za nje huku baadhi ya mashabiki wakiwa wanadhani ulikuwa umeingia ndani


Dk 74, Niyonzima anaachia fataki mpira unamgonga Manula, lakini anakimbia, anauwahi na kuudaka
SUB Dk 73 Haji Mwinyi anakwenda benchi, nafasi yake inachukuliwa na Geofrey Mwashiuya
Dk 72, krosi safi ya Domayo 'Chumvi', Afful anapiga kichwa safi hapa lakini Dida anadaka kwa umahiri hapa
Dk 70 sasa, Azam FC wanaonekana kuwabana Yanga na kuwafanya wacheze kama wanavyotaka wao ambao wana mabao mawili
SUB Dk 65, Samuel Afful anaingia kuchukua nafasi ya Yahya Mohammed, wote hawa ni raia wa Ghana
Dk 65, Yanga wanalalamika hapa baada ya Yahaya kuushika mpira, lakini mwamuzi anasema twende, cheza mpira
SUB Dk 61, Yanga wanamtoa Justine Zulu, nafasi yake inachukuliwa na Said Juma 'Makapu'


Dk 61, Azam wanaingia vizuri hapa, krosi ya Kapombe, Mahundi anaachia fataki hapa, goal kick
Dk 60, pasi ya Kamusoko, Emmanuel Martin anageuka vizuri hapa na kuachia fataki lakini haikulenga lango
Dk 58 sasa, Yanga wanaonekana kuchanganyikiwa na presha iko juu. Wanakuwa na papara na kupoteza utulivu
GOOOOOOOO Dk 54, Yahaya Mohamed anaruka juu na kuunganisha kwa kichwa krosi safi ya Sure Boy mbele ya Dante na mpira unapita Dida na kujaa wavuni


Dk 53, Yanga wanagongeana vizuri kabisa hapa, lakini Martin anapiga shuti mtoto na Martin anadaka kama nyanya hapa
Dk 49, mpira safi wa adhabu wa Juma Abdul, Aggrey anapiga kichwa hapa, inakuwa kona, Yanga wanachonga lakini mpira unaishia mikononi mwa Manula
KADI Dk 48, Gadel Michael analambwa kati ya njano kwa kumuangusha Msuva mara ya pili ndani ya sekunde 35
Dk 47 sasa, bado mchezo unakwenda taratibu na mpita unachezwa zaidi katikati ya uwanja
Dk 45, mpira unaanza na Azam FC wanakuwa wa kwanza kufika katika lango la Yanga, lakini si shambulizi kali


MAPUMZIKO
-Bocco anaingia tena, Yondani anapiga kichwa lakini wanachanganya hapa na Dida anautoa nje
-Bocco anaingia vizuri anaachia mkwaju hatariii, Dida anapangua hapa

DAKIKA 2 ZA NYONGEZA
Dk 45, Azam FC wanaonekana kuupoza mpira wakiwa wamepania kurejea mapumziko na bao moja
Dk 43 Sure Boy anawatoka Dante na Yondani, anaingia vizuri akiwa yeye na Dida anashindwa kufunga
Dk 40, Bocco anaingia na kuachia shuti kali lakini Dida anapangua safi unamtika anadaka tena
Dk 36, Msuva anaingia na kujaribu lakini wapi


SUB: Dk 36, Yanga wanamtoa Juma Mahadhi na nafasri yake inachukuliwa na Emmanuel Martin
Dk 34, krosi nyingine ya Niyonzima lakini Manula anapangua vizuri


Dk 31, Sure Boy anaonekana kutawala zaidi katika eneo la kiungo akishirikiana vizuri na Yakubu Mohamed na Mahundi Dk 29, Yanga wanafanya shambulizi jingine lakini Azam FC wanaonekana kuwa makini
Dakika ya 20: Mchezo unaendelea kwa kasi, Azam leo wanaonekana kuwa vizuri zaidi uliko mechi zilizopita.

Dakika ya 10: Yanga wanapambana kusawazisha bao.

Dakika ya 9: Msuva akosa bao baada ya kugongeana vizuri na Tambwe.

Dakika ya 7: Yanga wameanza kwa kuumiliki mpira 

Dakika ya 5: Mchezo unaendelea, timu zote zinasomana.


GOOOOOOOOOO: Dakika ya 2: Azam wanapata bao mfungaji ni John Bocco, kulitokea kutegeana kwa wachezaji wa Yanga, likapigwa shuti kipa wa Yanga, Dida akapaungua Bocco akaumalizia wavuni.

GOOOOOOOOOOOOOOOOO
Mpira umeanza kwa kasi ikionekana Azam FC wamepania kupata bao la mapema Dakika ya kwanza mchezo ndiyo umeanza, bado ni 0-0.  

1 COMMENTS:

  1. babu nataka kuona mecha ya azam na yanga leo kwa internet nipe link msaada

    ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV