February 5, 2017


Baada ya kutupia bao safi kabisa katika mechi dhidi ya Majimaji, mshambuliaji nyota wa Simba, Laudit Mavugo amesema anaweza kufunga mabao mengi zaidi na hilo anajiamini.

Mavugi amesema kwa ushirikiano ndani ya Simba, ataweza kufunga au kusaidia upatikanaji wa mabao kama ataendelea kupata nafasi.

“Kuna vitu nahitaji kuzoea, lakini ninahitaji kuendelea kucheza ili nizoee. Kufunga nitafunga tu zaidi. Nikishindwa nitatoa pasi wenzangu wafunge,” alisema.

Mavugo alifunga bao la tatu wakati Simba ikiitwanga Majimaji kwa mabao 3-0 mjini Songea, jana.


Kwa bao hilo la jana, Mavugo amefikisha mabao matano ya Ligi Kuu Bara.

Mshambuliaji huyo aliyejiunga na Simba kutoka Vital'O ya Burundi, amekuwa akionyesha kiwango kizuri lakini tatizo kwake limekuwa ni ufungaji wa mabao tu. 

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV