February 5, 2017


Mshambuliaji wa Yanga, Obey Chirwa amesema anaamini anaweza kuendelea kufanya vizuri lakini hofu yake ni moja tu.

Chirwa raia wa Zambia, amesema hofu yake kubwa ni majeruhi tu lakini vinginevyo anaamini anaweza kufanya vema zaidi.

“Shida ni maheruhi, kama nitakuwa katika hali nzuri, nikaendelea kucheza. Nina imani nitafanya vizuri,” alisema.

Chirwa amefunga mechi mbili mfululizo huku akionyesha uwezo mkubwa katika katika ufungaji.

Wakati anatua nchini akitokea Platinums ya Zimbabwe, kulikuwa na matumaini makubwa atafanya vizuri.


Lakini baadaye alianza kuonyesha cheche lakini baadaye akaanza kuyumba na kutofunga hali iliyozua mjadala kwamba ameshindwa kuonyesha cheche. 

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV