February 8, 2017



Paul Makonda


Makonda ametaja orodha ya majina kadhaa marufu kati ya 65 aliyodai kuwa anayo katika orodha yake ya wanaotakiwa kufika kituoni hapo kwa ajili ya zoezi hilo la mahojiano katika kampeni yake ya kuendeleza kupambana na utumiaji na biashara ya madawa ya kulevya.



Kati ya watu aliowataja ni Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji ambaye amesema ni kati wanatakiwa kufika ili kwenda kutoa maelezo kwa lengo la kuisaidia Polisi.

"Pia Kaka yangu Manji, pia naye ninamuomba afike," alisema.


Akizungumza na waandishi wa habari kwenye ofisi zake leo jijini Dar, Makonda alimtaja Manji kuwa anatakiwa kufika kituoni hapo Ijumaa hii, pia alimtaja mbunge wa zamani wa Kinondoni, Iddi Azzan ambaye alikuwa kipa wa timu ya wabunge na timu ya wabunge wa Simba wakati alipokuwa mbunge.

Majina mengine maarufu yaliyopo katika orodha hiyo ni na mfanyabiashara maarufu wa nguo, Hussein Pambakali, Mbunge wa Hai, Freeman Aikaely Mbowe, Mchungaji Josephat Gwajima.




Ameielezea orodha hiyo kuwa ni ya wale ambao wanahisishwa na biashara hiyo haramu na wengine wana taarifa muhimu zinazoweza kuwasaidia polisi kuwatia nguvuni vinara wa biashara hiyo.

Watu hao watahojiwa na polisi kama ilivyofanyika kwa watu waliotajwa kwenye orodha ya kwanza iliyohusisha pia mastaa wa muziki na filamu.


Wengine wanaohitaji ni pamoja na wamiliki wa Slipway na Yatchy Club. 


Orodha ya awamu ya pili ya Makonda ina jumla ya majina 65.

8 COMMENTS:

  1. Duh siyo mchezo. Ila kwa Manji halo nafikiri amefanya mengi kWa taifa letu!.

    ReplyDelete
  2. Duh orodha hiyo so mchezo. Ila kuna wengine duuu inatia mashaka kidogo. Kama Mahesh. Manji kwa jinsi anavyoisaidia jamii kubwa ya watanzania namuombea tuhuma hiz hizi zisiwe za kweli juu yake

    ReplyDelete
  3. Duh orodha hiyo so mchezo. Ila kuna wengine duuu inatia mashaka kidogo. Kama Mahesh. Manji kwa jinsi anavyoisaidia jamii kubwa ya watanzania namuombea tuhuma hiz hizi zisiwe za kweli juu yake

    ReplyDelete
  4. huyo makonda ni simba .pesa alizonazo manji au freenan mbowe kwanini wafanye biashara ya unga. itawasaidia nini. wakati yeye ndie mbeba unga na jamaa zake. makonda ni bwege tu anaficha mambo yake

    ReplyDelete
  5. The war against drugs must be conducted in a Good Way especialy for leaders (tops)

    ReplyDelete
    Replies
    1. Well Said ! but should not spoil the name of person who has done great things for YANGA.

      Delete
  6. Kwa mchango mkubwa Manji anaotoa kwa jamii jamani ameajiri maelfu ya watu hizi tuhuma zinamchafulia jina na kumharibia biashara.Na biashara ikiharibika familia nyingi zitaathirika na hii ni kwa sababu wengi ndo wanapata riziki zao kwenye kampuni zake.Sidhani kama tuhuma hizi zina ukweli ukizingatia kwamba yeye ni mfanyabiashara iweje leo afanye jambo la kumchafulia jina na kuharibu biashara zake?!!!

    ReplyDelete
  7. Yusuf, I would say is most amazing and dynamic personality I have come across ever. Very humble and down to earth. Very focused on his Business. Loves Tanzania and Tanzanians and always thinks for the betterment of Society. This seems to be conspiracy to defame him for benefit of some unnamed personalities. I am confident he will come out as winner over all the evils plotted. #iSupportYusufManji

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic