February 15, 2017


PSG imeonyesha inaweza baada ya kuitwanga Barcelona kwa mabao 4-0 katika mechi ya kwanza ya hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mbaingwa Ulaya.


Barcelona ikiwa ugenini jijini Paris imeshindwa kuonyesha cheche licha ya kuongozwa na nyota wake Lionel Messi na Neymar na kujikuta ikipokea kipigo hicho cha kondoo mchovu.

Angelo Di Maria ametumbukia nyavuni mara mbili huku Endson Cavani aliyetimiza miaka 30 jana akifunga moja na Julian Draxler akifunga moja.


Mechi nyingine Benfica imeifunga Borussia Dortmund kwa bao 1-0.0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV