February 25, 2017



Kocha wa zamani wa Simba, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ amesema Yanga haina jeuri ya kuifunga timu yake hiyo ya zamani katika mchezo wao wa leo Jumamosi kwani Wekundu wa Msimbazi wana kikosi imara.

Julio amesema huko nyuma Yanga iliinyanyasa Simba kwa kuwa haikuwa na kikosi imara kama ilivyo sasa, hivyo leo ushindi kwao ni jambo la kawaida.

Simba inaongoza ligi ikiwa na pointi  51 katika mechi 22 ikifuatiwa na Yanga yenye pointi 49 katika michezo 21. Timu hizo zinakutana leo Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Akizungumza na Julio alisema kuwa, Simba ni lazima ishinde ili kudhihirisha uwezo wa timu yao na dhamira ya kutwaa ubingwa wa ligi msimu huu.

 “Simba lazima wawe mabingwa msimu huu kuhakikisha tunashinda Jumamosi (leo), timu inacheza vizuri na wachezaji wanacheza kitimu  hivyo Yanga wasahau suala la kutwaa ubingwa msimu huu. “Kuhusu ligi ya safari hii haina ushindani mkubwa kwani timu hazina fedha za kutosha kwani zile za wadhamini hazijitoshelezi hivyo kusababisha timu nyingine kushindwa kufanya vizuri,” alisema Julio.

“Ni Simba na Yanga labda na Azam ndizo zinazoonyesha upinzani wa haki lakini hizo nyingine zilizobaki ni kama zinajikongoja tu kwani hazina uwezo wa kupambana na vigogo hao."

SOURCE: CHAMPIONI



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic