February 14, 2017Pamoja na ushindi mnono, Kocha wa Yanga, George Lwandamina amesema kamwe hawatawadharau Ngaya katika mechi ya marudiano.

Yanga imeitwanga Ngaya kwa mabao 5-1 kwao Moroni katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya awali.


Lwandamina raia wa Zambia amesema lazima wafanye vizuri zaidi na atapanga kikosi imara.


"Bado hatujavuka, hatuwezi kufanya mzaha. Tunahitaji kucheza na kushinda tena," alisema.


Pamoja na juhudi za Ngaya kutaka kujitutumua lakini walionekana kuushindwa mziki wa Yanga.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV