Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa amesema wao wanaamini watani wao, Simba walimjua mwamuzi Mathew Akrama angechezesha mechi yao ya kesho.
Lakini walikaa kimya na jambo hilo wanaliona si sahihi lakini wamewataka mashabiki wao kwenda uwanjani wakiwa watulivu na washangilie kiistaarabu.
“Tunajua kuwa Simba walijua kuhusiana na Akrama. Lakini mashabiki hawana haja ya kuwa na hofu.
“Waende uwanjani kwa wingi, waishangilie timu yao na sisi tunachotaka ni mwamuzi kuchezesha kwa haki na kufuata sheria 17 za soka,” alisema Mkwasa.
Akrama wa Mwanza ndiye ametangazwa kuuchezesha mchezo huo unaosubiriwa kwa hamu na mashabiki wa soka nchini.
Washafungwa yanga tayari
ReplyDelete