Yanga wamesema wanashangazwa sana na watani wao Simba kuonekana wako 'busy' na mechi ya kesho utafikiri baada ya hapo wanatangazwa mabingwa.
Mmoja wa wajumbe wa kamati ya utendaji ya Yanga amesema, wanaamini watawafunga nyingi Simba kutokana na presha yao.
"Hawa jamaa wanajipa pesha sana nakuambia, unajua ungebahatika kwenda kwenye kambi ya Yanga ungeshangaa sana.
"Watu wako kikazi na hakuna presha. Wachezaji wanaendelea na mambo yao vizuri na hakuna presha kabisa. Sasa wenzetu sijui wana nini, utafikiri wakishinda kesho, wanatangazwa mabingwa na kupewa kombe!" alisema.
Mechi hiyo itakayopigwa kesho kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, inaonekana kuzidi kuwa na presha huku kila upande ukiogopa kupoteza.
0 COMMENTS:
Post a Comment