February 24, 2017


Kikosi cha Simba kimerejea jijini dar es Salaam na kujichimbia katika Hoteli ya kisasa ya Sea Scape.

Hoteli hiyo iko eneo la Mbezi Beach, mpakani na Kunduchi na ni moja ya hoteli mpya za kisasa karibu kabisa na ufukwe wa Bahari ya Hindi.


Simba ndiyo watalala hapo siku mbili wakianza na leo, siku moja kabla ya kuwavaa watani wao Yanga kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na baada ya hapo kesho baada ya mechi hiyo.

Kabla, Simba walikuwa mjini Zanzibar ambako waliweka kambi ya siku kadhaa kujiandaa na mechi hiyo.









0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic