February 6, 2017Kocha wa muda wa Azam FC, Idd Nassor Cheche, ameibuka na kusema kuwa, licha ya kuuanza vizuri mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara, lakini itakuwa ngumu kwao kuwa mabingwa.
Cheche amesema licha ya kuwa na wakati mgumu wa kutwaa ubingwa, lakini watahakikisha lazima nafasi ya pili waichukue wao.

Azam ambao kabla ya mchezo wao wa jana Jumapili dhidi ya Ndanda walikuwa wanashika nafasi ya nne wakiwa na pointi 34, wameachwa pointi 15 na vinara Yanga.

Cheche alisema ushindani wanaoupata kwenye ligi kwa sasa ni mkubwa huku presha kubwa ikiwa ni namna ya kufanya ili waweze kuwashusha walio juu yao.

“Tunataka kumaliza nafasi ya juu zaidi ya hii tuliyopo sasa, suala la ubingwa litakuwa gumu kutokana na kasi ya wapinzani wetu ilivyo.

“Lakini tunajipanga zaidi kuhakikisha nafasi ya pili hatuikosi, tunaitaka nafasi hiyo kwa lengo la kumaliza ligi kwa heshima na si kingine,” alisema Cheche.

SOURCE: CHAMPIONI


3 COMMENTS:

  1. Idd Cheche akiri, sio akili! Kiswahili gani hicho kibovu hivyo?

    ReplyDelete
  2. Nafasi ya pili mkipata basi arsenal atakuwa bingwa epl

    ReplyDelete
  3. Nafasi ya pili mkipata basi arsenal atakuwa bingwa epl

    ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV