February 4, 2017Simba inashuka kuivaa Majimaji ikiwa na pengo la pointi 4 dhidi ya watani wake, Yanga.


Inachotakiwa ni kushinda na kubakiza pengo la pointi moja, usisahau Majimaji wako nyumbani.


Kabla ya kuivaa Majimaji, kiungo mwenye kasi wa Yanga na kinara wa ufungaji wa mabao hadi sasa, Simon Msuva amewapa maneno yake.


Msuva amewapa tahadhari Simba kwa kusema, endapo mechi yao na Majimaji watapoteza, basi wafute kabisa ndoto za kuwania ubingwa wa ligi kuu msimu huu.


Yanga kwa sasa ndiyo inayoongoza ligi hiyo kwani kabla ya mechi ya jana ilikuwa na pointi 46 mbele ya Simba yenye 45, halafu nafasi ya tatu ipo Kagera Sugar yenye pointi 37 kisha Azam FC ni ya nne na pointi 34.

Msuva alisema wamejipanga kuhakikisha wanapata ushindi katika kila mchezo wao jambo ambalo litawafanya kuchukua ubingwa kirahisi.


“Kikosi chetu kipo salama kiasi kwamba tunachowaza sasa ni kuendelea kushinda kila mchezo ili tuweze kutwaa ubingwa kwa mara nyingine tena, tunajua tuko kileleni kwa zaidi ya pointi moja, hatutaki kushuka.


“Simba wameenda kucheza Songea na si rahisi kwao kupata ushindi, ninachoweza kuwaambia ni kwamba wajue kuwa wakizidi kuteleza tu basi safari yao itakuwa imeishia hapo, hawawezi kuwa mabingwa,” alisema Msuva mwenye mabao tisa katika ligi kuu kabla ya mechi ya jana.

SOURCE: CHAMPIONI

1 COMMENTS:

  1. Reading between the line ni kama anatoa msukumo Simba ishinde

    ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV