February 1, 2017Muda ukiwa unahesabika kuelekea mchezo wao dhidi ya Simba, Kocha Mkuu wa Majimaji, Muingereza, Kally Ongala amesema haoni sababu ya kushindwa kuifunga Simba kwa kuwa wapo katika hatari ya kushuka daraja.


Simba ambayo inashika nafasi ya pili ikiwa na pointi 45 nyuma ya vinara wa ligi hiyo Yanga wanaoongoza kwa pointi 46, Jumapili hii inatarajia kucheza na Majimaji mkoani Songea kwenye Uwanja wa Majimaji ambapo kwa sasa  wapinzani wao hao wanakamata nafasi ya 14 wakiwa na pointi 20.


Akizungumza Ongalla alisema kutokana na kutopata muda mrefu wa kufanya maandalizi yao hawana sababu yoyote ya kushindwa kuifunga Simba kwa kuwa wapo kwenye wakati mgumu.


"Kiukweli tunashukuru tunaendelea na maandalizi kwa kuwa muda umekuwa wa kutosha hivyo tutahakikisha tunaifunga Simba kwa sababu hatupo katika nafasi nzuri hivyo ushindi kwetu ni kitu muhimu.“Unajua Simba ni timu nzuri kwa sababu hata ukiangalia wapo katika nafasi nzuri kwenye msimamo tofauti na sisi, sasa hilo hatutaki kulipa nafasi kwa kuwa tunachokiangalia ni suala la matokeo hivyo wao wajue kuwa lazima huku watuachie pointi tatu," alisema Ongalla.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV