February 14, 2017Kama ulikuwa unaamini Mtibwa Sugar sasa wameporomoka, basi unajidanganya sana.

Hayo ni maneno ya Msemaji wa klabu hiyo, Thobias Kifaru ambaye anasema kufungwa mabao 5-0 dhidi ya Mbao FC, haina maana wameporomoka.

“Watu hawajui katika soka pia kuna matokeo ya kushangaza. Imetokea kwetu Mtibwa lakini inaweza kutokea kwa mwingine yoyote.

“Lakini Mtibwa Sugar bado iko imara, kiwango chetu ni bora na tutaendelea kupambana kwa ushindani katika ligi kuu,” alisema.

Kifaru alisema wamelichukuliwa suala lile kama mafunzo lakini wanashangazwa na watu kulivalia njuga kama hakuna timu iliyowahi kufungwa mabao hayo katika ligi kuu.


“Makocha wanaendelea na kazi ya mechi nyingine, si ile iliyopita.”

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV