February 14, 2017Kampuni ya StarTimes Tanzania, leo Jumanne inatarajiwa kusherehekea Siku ya Wapendanao sambamba na wateja wao kupitia promosheni yao ya Ni Valentine’s na StarTimes.

Promosheni hiyo iliyoendeshwa kwa takribani mwezi mmoja, ilihitimishwa kwa kupatikana washindi 15 kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania ambao waliitumia siku ya jana kula chakula cha usiku na kulala kwenye hoteli za kifahari zilizopo sehemu mbalimbali wakiwa na wapenzi wao.

Akizungumza wakati wa hafla ya kuwapongeza washindi hao, Meneja Masoko wa StarTimes, Felix Awino, amesema: “Tunayo furaha kubwa ya kusherekea Siku ya Wapendanao tukiwa karibu na wateja wetu.


"Promosheni yetu hii ya Ni Valentine’s na StarTimes ambayo imetupatia washindi hawa, ni sehemu ya kuwajali wateja wetu na tunawaahidi tutawafanyia mengi makubwa kila siku.”


Awino aliongeza kuwa, washindi hao kwa kila mkoa, wataenda kujumuika na wapenzi wao katika hoteli za Seascape ya jijini Dar, Malaika (Mwanza), Usungilo (Mbeya), Palace (Arusha) na Morena (Dodoma).


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV