February 24, 2017Huku utata wa mshambuliaji wa Yanga, Donald Ngoma kucheza au kutocheza katika mchezo wa kesho dhidi ya Simba ukiendelea, Kocha wa Yanga, George Lwandamina ametoa tamko juu ya mchezaji huyo.


Ngoma anasumbuliwa na majeraha ya goti, lakini viongozi wa Yanga wamekuwa wakifanya juu chini kuhakikisha mchezaji huyo anakuwepo katika mchezo huo wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa kwenye raundi ya pili.


Kwa siku kadhaa sasa Ngoma amekuwa akifanya mazoezi ya peke yake katika gym akisimamiwa na mtaalam mwanamke, ameshindwa kuungana na wenzake walipo kambini tangu Jumatatu kutokana na matatizo yanayomsumbua.


“Siwezi kusema kama Ngoma atakuwepo au la, hiyo kazi nimewaachia madaktari ambao ndiyo watanipa jibu kamili kabla ya mchezo,” alisema Lwandamina na kuongeza:


“Lakini kama ikitokea tukamkosa wala haina shida kwa sababu haitaathiri kikosi changu kwa maana kwamba tulimkosa huko nyuma na tumefanya vizuri tu.“Tunajiandaa vizuri kwa ajili ya mchezo wetu dhidi ya Simba, kikosi kipo kwenye hali nzuri na hakuna shida yoyote.”

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV