February 3, 2017


Straika wa Simba, Juma Liuzio, amesema wamejua tatizo lililopo katika kikosi chao na sasa wanajipanga kufanya kweli katika mchezo wao dhidi ya Majimaji.


Liuzio amesema tatizo kubwa katika kikosi chao ni umaliziaji, akidai wanatengeneza nafasi nyingi lakini umaliziaji ndiyo mbovu, sasa wameufanyia kazi na wataanza kuonyesha mabadiliko hayo katika mechi ya Majimaji.


“Sidhani kama Simba ni timu mbovu kama watu wanavyofikiri, nikwambie kitu, sisi washambuliaji tungekuwa makini mechi na Azam, basi matokeo yasingemalizika yale ya kufungwa bao 1-0.


“Kiukweli, viungo wetu walitutengenezea nafasi nyingi za kufunga lakini umakini wetu mbaya ndiyo ukasababisha sisi tupoteze mchezo huo.“Tumeliona hilo tatizo letu, niwaahidi mashabiki wa Simba kuwa, tatizo hilo tumelimaliza na mechi dhidi ya Majimaji tutathibitisha hilo,” alisema Liuzio.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV