MPIRA UMEKWISHA
DAKIKA 2 ZA NYONGEZA
Dk 89 Zimbwe anaingia vizuri lakini pasi yake inaokolewa na kuwa kona. Inapigwa hakuna kitu
SUB Dk 86, Mavugo anakwenda nje na nafasi yake inachukuliwa na Pastory Athanas
Dk 84, Kichuya anaachia mkwaju, hatari lakini kipa anadaka vizuri kabisa
Dk 84, Mo Ibrahim anaunganisha krosi , mpira wa kichwa unagonga mwamba hapa
Dk 83, Abdallah Mguhi anaingia kuchukua nafasi ya Rehani upande wa Lyon. Mguhi ndiye aliyeifunga Simba katika mechi ya Ligi Kuu Bara mzunguko wa kwanza (leo ni mechi ya Kombe la Shirikisho)
Dk 82 Cosmas Lewis anapiga shuti kuuubwa akiwa na nafasi
Dk 76, Kichuya aanachia shuti kali lakini kipa anaonyesha kazi nzuri na kupangua
Dk 75, Lyon wanaingia vizuri lakini mpira wa Mwalyanzi unakuwa mrefu
Dk 72, Mavugo anatoa pasi nzuri kwa Mo Ibra lakini anaachia shuti kaaalii
SUB Dk 70, Mohamed Ibrahim ameingia kuchukua nafasi ya Ndemla
Dk 66, bado mpira unachezwa katikati ya uwanja. lakini Simba wanahitahidi kuingia langoni mwa Lyon mara nyingi zaidi
Dk 62, mpira wa faulo wa Kotei unatoka juu sentimeta chache juu ya lango la Simba
KADI Dk 61, Miraji Adam analambwa kadi ya njano kwa kumuangusha Ajibu
Dk 58, Laudit Mavugo anaiandikia Simba bao baada ya kupiga shuti dhaifu la chinichini na kujaa wavuni
Dk 52, mpira unachezwa taratibu kabisa katika ya uwanja na Lyon wanaendelea kujilinda zaidi
Dk 45,mpira umeanza lakini kuna mchezaji wa Lyon ameumia pale
MAPUMZIKO DAKIKA 2 ZA NYONGEZA
Dk 45, Simba wanagongeana vizuri hapa lakini shuti la Mavugo linapaa juuuuuuuDk 42, krosi maridadi ya Bukungu lakini kipa wa Lyon tena anaonyesha umahiri na kuupiga ngumi vizuri kabisa
Dk 40, Zimbwe anaangushwa zi mbali sana na lango la Lyon
Dk 39, Mavugo anawachambua Lyon na kutoa pasi ya kisigino kwa Ajibu lakini shuti lake linaokolewa
Dk 38, Ajibu anawachambua mabeki wa Lyon, katikati ya msimu lakini anabutuaaaa shuti buuuuu
Dk 36, nafasi nzuri kwa Simba lakini Ndemla anavuruga na mpira unaokolewa. Angeweza kuwapa pasi wenzake lakini akawa na papara
Dk 35, Simba wanafanya shambulizi tena, lakini Lyon wanaokoa na kuwa kona, inachongwa na kupigwa lakini inaokolewa
Dk 34, Mkude anaachia mkwaju mkali kabisa hapa, lakini kipa anaokoa kwa umahiri kabisa
Dk 32, mchezaji wa Lyon yuko chini hapa
Dk 30, mpira wa adhabu wa Ajibu unagonga ukuta na kutoka nje
Dk 27 Ajibu anaingia vizuri kabisa lakini shuti lake halikulenga lango
Dk 22, mpira unachezwa katikati zaidi huku Lyon wakijilinda zaidi na mashambulizi ya Simba, si makali
Dk 15, mechi bado ngumu lakini Simba ndiyo wanaoshambulia zaidi
Dk 30, mpira wa adhabu wa Ajibu unagonga ukuta na kutoka nje
Dk 27 Ajibu anaingia vizuri kabisa lakini shuti lake halikulenga lango
Dk 22, mpira unachezwa katikati zaidi huku Lyon wakijilinda zaidi na mashambulizi ya Simba, si makali
Dk 15, mechi bado ngumu lakini Simba ndiyo wanaoshambulia zaidi
Dk 10, krosi safi ya Liuzio inakosa mtu na inaonekana Lyon wanafanya mashambulizi ya kushitukiza
Dk 5, Juma Liuzio anaingia vizuri lakini anaangushwa
Dk 1 Mechi imeanza kwa kasi, Simba wanashambulia mfulilizo
0 COMMENTS:
Post a Comment