February 26, 2017

Mashabiki wa Simba, jana walimpokea kwa shangwe aliyekuwa mgombea wa Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Lowassa.

Mashabiki hao walionyesha shangwe kubwa baada ya Lowassa kuingia Uwanja wa Taifa wakati wa mechi ya watani Simba dhidi ya Yanga, jana.

Wakati akiwa jukwaa kubwa aliwapungia mkono, nao wakamshangilia kwa nguvu.


Hata upande wa Yanga, nao walionyesha shangwe kuu na kumpokea Lowassa huku baadhi yao wakizungusha mikono kuonyesha hali ya mabadiliko.

Lowassa aliongozana na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na msanii Wema Sepetu ambaye amejiunga na chama hicho hivi karibuni akitokea akitokea chama tawala cha CCM.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV